Thailand

Binti wa Mfalme ahudhuria sherehe za miaka mia mbili Bangkok

Huko Thailand, Familia ya Kifalme iliwakilishwa na Binti wa Mfalme Soamsawali katika sherehe za miaka mia mbili zilizofanyika katika Senta ya Kibahá’í Bangkok. Ratiba ya jioni iliambatana na muziki, sala, na dansi za kitamaduni za Kithai. Mkusanyiko huo ulihudhuriwa na karibia watu 250 na ulikua ni mmojawapo wa mikusanyiko mingi iliyofanyika katika nchi leo.