Makao Makuu ya Kibahá'í

Hema la Bahá’u’lláh lawekwa Bahji

Katika tukio la kusherehekea miaka mia mbili katika Nchi Takatifu, mojawapo ya hema ambapo Bahá’u’lláh aliishi, liliwekwa kwenye ardhi ya Bahji kwa ajili ya mahujaji na watembeleaji. Kufuatia kuondoka kwa Bahá’u’lláh kutoka mji mkongwe wa ‘Akká mwaka 1877, hema liliwekwa kwa ajili yake katika matukio tofauti. Mahema hayo yaliuwezesha kupata hifadhi wakati wa matembezi Yake mashambani na kwa wakati mwingine yaliwekwa karibu na mahali ambapo Bahá’u’lláh alikaa ili aweze kuwapokea mahujaji na wageni. Hema hili lilitumwa kwa Bahá’u’lláh kama zawadi kutoka India katika kipindi hicho.