India

Huko India, sherehe za miaka mia mbili zahamasisha matendo ya huduma na sadaka

Matendo ya huduma yalitolewa India kuenzi sikukuu za miaka mia mbili. Huko Sambalpur, kikundi cha vijana chipukizi waliandaa kuangalia sickle cell, makundi ya damu na msukumo wa damu kwa wakazi wake, hususani wamama. Huko Agartala, Baraza la Kiroho la Kijiji liliandaa eneo la kujitolea damu na kila mtu alipanda miti na kusafisha mitaa ya miji.