Kiribati

Jua kuchwa kuashiria mwanzo wa sherehe za miaka mia mbili

Wakati jua likizama huko Pasifiki, tamasha la sherehe za kuzaliwa kwa Báb and Bahá’u’lláh limeanza. Katika kipindi hiki cha kihistoria cha kuashiria miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh, sherehe za mamilioni zitafanyika ndani ya masaa 72 ulimwenguni kote, kuanzia machweo ya kwanza hadi ya mwisho, na kumalizika Hawaii tarehe 22 October.