Uganda

Kwaya ya Uganda wakiimba sala katika Hekalu

Ee Mungu wangu! Ee Mungu wangu! Unganisha mioyo ya watumishi Wako, na uwafunulie kusudi Lako kuu. Waweze kufuata amri Zako na kudumu katika sheria Yako. Uwasaidie, Ee Mungu, katika jitihada yao, na uwajalie nguvu kukutumikia Wewe. Ee Mungu! Usiwaache peke yao, bali uongoze hatua zao kwa nuru ya maarifa Yako, na ufurahishe mioyo yao kwa upendo Wako. Hakika, Wewe ndiye Msaidizi na Bwana wao.