Wajumbe wa kabila la Kiriri, kabila la asili huko Brazili mashariki, walienzi maadhimisho ya miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bahá’u’lláh kwa sherehe maalum ya Toré- desturi ambayo jamii hukutana kwa pamoja kwa furaha na heshima ya hali ya juu kuungana na wahenga wakale kupitia sala na nyimbo.