Australia

Sherehe ya kusisimua katika wodi ya hospitali

Huko pwani ya mbali ya Kaskazini mwa New South Wales, Australia, Mbahá’í mzee sana alilazwa wiki chache kabla hajafariki. Wakati tarehe za kuadhimisha miaka mia mbili, mgonjwa na familia yake waliamua kusherehekea wakiwa hospitali. Waliongea na wafanyakazi wa hospitali, wakijumuika nao katika sala na umuhimu wa tukio hili na wagonjwa wengine, na kwa msaada wao, walifanya maandalizi ya mkutano wa heshima kabisa wodini. Roho ya tukio hilo iliinua mioyo ya wafanyakazi wote, wagonjwa, familia na marafiki. Wodi ya hospitali ilijaa maua na sherehe hiyo ndogo ilifunguliwa kwa sala ya ‘Abdu’l-Bahá kwa Kiajemi, iliyoimbwa vizuri na mgonjwa mwenyewe.