Malawi

Shule ya Bambino yaandaa sherehe ya watu 1,000

Wiki moja ya mawasilisho ya wanafunzi ilifikia mwisho wake katika sherehe za miaka mia mbili ya Bahá’u’lláh zilizofanyika shuleni, zilifanywa na wazazi na viongozi wa kijiji. Zaidi ya watu 1,000 walihudhuria maadhimisho katika shule ya Bambino, Lilongwe, Malawi. Kikundi cha walimu wa shule waliandaa sherehe iliyodumu wiki moja, iliyoanza kwa mawasilisho kutoka kwa wanafunzi juu ya Bahá’u’lláh. Walimu walijitolea kuandaa sherehe za miaka mia mbili kwa ajili ya shule yao baada ya kujifunza juu ya maisha ya Bahá’u’lláh. Shule ya Bambino yenye wanafunzi 800 ni moja ya shule nyingi zilizohamasishwa na jitihada za kijamii na kiuchumi za ki-Bahá’í, nyingi zikiwa katika eneo la elimu.