Uzbekistan

Wageni 180 wajiunga na sherehe Tashkent

Mji ambao - zamani ulikua ni kituo cha biashara katika barabara ya hariri ya kale - mji mkuu wa Uzbekistan. Ni mji wenye misikiti na makanisa, na njia nzuri, yenye maeneo ya kukaa yenye kukaribisha na chemchem. Utamaduni wake- ulioundwa na miaka 2000 ya historia- ulioneshwa na ukarimu ambao wageni huwa marafiki mara moja. Bila shaka, jamii ya Wabahá’í walianza sherehe za mchana kwa kukaribisha chakula cha kiasili cha Uzbek 'plov', mchanganyiko wenye harufu nzuri wa mchele,karotu, vitunguu na nyama unaopikwa kwenye moto. Ratiba ilijumuisha kutizama filamu ya *Mwanga wa Dunia*. Kilichoonekana zaidi kwa waliohudhuria ni jamii yenye vijana na jinsi vijana wadogo walivyofanya kazi kwa pamoja na watu wazima kwa roho ya urafiki, wengine walivutiwa na maelezo ya maisha ya Bahá’u’lláh na Mafundisho Yake na waligundua Maandiko yake dhana walizoweka muda mrefu katika mioyo yao.