Taarifa ya habari kuhusu sherehe za mahali Taarifa ya habari ya hivi karibuni ya televisheni kwa lugha ya Kifaransa imeelezea sherehe za miaka mia mbili zilizofanyika kwenye ujirani kadhaa huko Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kuelekea kwenye sherehe za Siku Kuu za jiji zima. Kati ya picha za video za kuimba na kucheza, kuna mahojiano na waliohudhuria ambao wanaongelea kuhusu matokeo ambayo ujumbe wa Báb unao kwenye maisha yao.