Likihuishwa kwa masimulizi ya hadithi, kongamano lenye kuchangamsha launganisha watu 3,000 katika maandalizi ya sherehe ya miaka mia mbili Matukio dhahiri kutoka maisha ya Báb yalisimuliwa na vijana kwenye kongamano lililofanyika Bukavu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hadithi hizi zilichangia uwepo wa mandhari yenye kuchangamsha na ambayo inachochea fikra. Kwa washiriki hao 3,000, ilikuwa ni fursa nzuri ya kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu jinsi jumuiya zinavyojiandaa kusherehekea ipasavyo sherehe ya miaka mia mbili.