close

Muungano wa Madola ya Amerika

Ufungaji wa sanaa ulitumia mwanga kuonyesha umoja
Ikiitwa "750" mradi huu wa upiga picha wa ushirikiano uliwahusu wapiga picha 18 kutoka nchi tano na ulifanywa kuadhimisha mwaka wa sherehe za miaka mia mbili. Picha mia saba hamsini za mikono, kila mkono ukishikilia mshumaa, kwa ubunifu ulikumbusha mafundisho, kujitoa dhabihu, na kuuawa kwa Bab. Sanaa hii imeonyeshwa katika vyuo vikuu viwili, na utakuwa kwenye maonyesho katika Senta ya Ukaribishaji ya Nyumba ya Ibada, Wilmette, Amerika ya Kaskazini kutokea tarehe 28 Oktoba hadi tarehe 30 Novemba.