Australia yaitikia kipindi cha sherehe za miaka mia mbili kwa sherehe nyingi Wakati sherehe za miaka mia mbili zikifunguliwa huko Australia, watu pande zote za nchi wanakusanyika katika mikutano ya ibada kuipa sura hamu ya ndani ya kuwasiliana na Mungu. Maelfu wamekuwa wakija kwa pamoja katika Nyumba ya bara ya Kuabudu huko Sydney pamoja na nyumba pande zote za nchi kusali pamoja na kuelekeza ahadi zao za kuchangia katika maendeleo ya kimwili na ya kiroho ya jamii zao.
Hisia hizi za ibada zimeleta mpangilio wa kung'aa wa jitihada za kisanii, kutafakiri mchanganyiko wa tamaduni uliopo katika nchi. Watu wanatumia sanaa - kutoka maigizo hadi michoro ya rangi ya dhahania, kusimulia hadithi hadi maonyesho ya muziki - ili kuonyesha ushujaa wa waumini wa kwanza wa Bab na kuvuta hamasa kutokana na hadithi hizo. Jamii nyingine zimekuja kwa pamoja kutumia sanaa kupendezesha mazingira yao, wakiweka katika fikra matokeo ya mazingira katika maisha yao.
Wakiweka katika fikra malengo ya juu ya ujumbe wa Imani ya Kibahai, watu wanawakaribisha idadi inayoongezeka ya marafiki zao na majirani kujifunza kuhusu maisha na ujumbe wa Bab na Bahá’u’lláh. Na kama ilivyo kawaida katika sehemu nyingine duniani kote, mikusanyiko kutazama filamu Alfajiri ya Mwanga inawapa idadi kubwa ya watu nafasi ya kutafakari kuhusu ni nini maana ya kutoa ahadi katika maisha yao kubadilisha jamii.