close

Kenya

Maneno ambayo Báb Alimwambia Mullá Ḥusayn yanahamasisha utunzi wa muziki
Akiguswa na maneno ambayo Báb Alimwambia Mullá Ḥusayn, msanii mmoja kutoka Nairobi, Kenya, alitunga wimbo ulioitwa “Amka”. Wimbo huo unanukuu kutoka tamko lifuatalo la Báb kwa Mullá Ḥusayn, alipoambiwa kuwa hatamsindikiza Báb kwenda kuhiji Makka na Madina: “Inua wito: 'Amkeni, Amkeni, kwani tazama! Lango la Mungu liko Wazi, na mwangaza wa asubuhi unatawanya mng'aro wake juu ya jamii nzima ya binadamu! Yule Mwahidiwa amedhihirishwa; andaeni njia kwa ajili Yake, Enyi watu wa dunia! Msijinyime wenyewe neema yake inayookoa, wala kuufungia macho utukufu wake unaong’aa.'”