Hotuba ya mwisho ya Bab kwa waumini Wake wa mwanzo ilihamasisha wimbo huko Norway "Mashairi ya wimbo maarufu unaoimbwa mara kwa mara katika mikutano pande za Norway yaliyotolewa kutoka hotuba ya mwisho ya Bab kwa Herufi za Uhai, Wafuasi wake 18 wa kwanza ambao bila utegemezi wowote walimtambua Yeye kama Mtume wa Mungu mwaka 1844. ""Enyi Marafiki Wangu Wapendwa"" ikinukuu kutoka matamshi ya Bab kwa wafuasi wake wa mwanzo wakati akiteua kwa kila mmoja wao kazi maalum yenye lengo la kufikisha ujumbe Wake wa ufufuko kwa roho zitafutazo pande zote za Uajemi na zaidi.
*Enyi Marafiki Zangu Wapendwa! Nyinyi ni wabebaji wa jina la Mungu katika Siku hii. Inawapasa kila mmoja wenu kudhihirisha sifa za Mungu,...kila kiungo cha mwili wenu kinapaswa kushuhudia katika hali ya juu Hali ya juu ya kusudi lenu, uadilifu wa maisha yenu, ukweli wa imani yenu, na utukufu wa hali yenu ya ibada, Enyi marafiki Wangu wapendwa! Ninyi ni chumvi ya ulimwengu, walakini kama chumvi imepoteza ladha yake, Ni wapi itakolezwa? Kila kiungo cha mwili wenu...Eny marafiki Wangu wapendwa!"*