close

Australia

Maandiko ya Báb yalihamasisha ufundi ubunifu wa makaratasi kwa ajili ya tamasha la sanaa la jumuia
Mkusanyo wa vipande, vilivyoashiria umbo la binadamu, vilitengenezwa kwa ajili ya tamasha la sanaa huko Boroondara, Australia. Vipande hivyo vilitengenezwa kwa kukunja karatasi, mbinu iliyojumuisha kuviringisha na kuumba vipande vya karatasi kutengeneza miundo. Tukio la kijamii, likisherekea miaka mia mbili litajumuisha media tofauti, ikiwemo sanaa za maonyesho, muziki, maigizo na filamu.