close

Angola

Kituo cha Kibahá'í kujengwa tayari kwa ajili ya maadhimisho ya miaka mia mbili
Mji wa Cazombo, Angola, shehere zijazo za miaka mbili zilihamasisha jumuiya ya Kibahá’í kujenga kituo cha eneo, ambacho kingejumuisha vyumba vya ofisi, vyumba vya mikutano na maeneo ya kulala. Jumuiya nzima ilishiriki katika mchakato wa ujenzi, kujumuisha watoto na vijana. Kituo cha Kibahá’í kilimalizika kujengwa ndani ya muda kwa ajili ya maadhimisho, kikikaribisha zaidi ya watu 800 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Báb.