close

Jamhuri ya Afrika ya Kati

Sherehe zilzofanywa na familia na vikundi huku Jamhuri ya Afrika ya Kati
Maadhimisho ya sherehe za miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Bab yanaongeza kasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya baadhi ya familia na vikundi huko Bengui na Bimbo wakiitisha mikusanyiko ya furaha. Kwa hali ya ukarimu, ukaribu, mikusanyiko ilileta kwa pamoja idadi kubwa ya marafiki wao na jamaa katika kutolea heshima kumbukumbu ya maisha ya Bab. Matukio yaliambatana na maonyesho ya kisanii yalionyesha umuhimu wa ufunuo wa Bab.