close

Bermuda

Maadhimisho huanza
Katika kipindi hiki cha miaka mia mbili, jumuiya kote nchini Bermuda zinatafakari mchango wa kisiwa chao katika kujenga amani zaidi ulimwenguni. Kupitia eneo lake lote la ukubwa wa maili za mraba 19, watu husali pamoja, hupendezesha mazingira, huchota hamasa kwenye hadithi za wavunja-mapambazuko, na hupanga mipango kwa ajili ya kuboresha jumuiya zao. Vijana na watoto, hususani, wamekuwa wakija pamoja kutafakari wajibu wao muhimu kwa kizazi chao wa kuchangia kwenye maendeleo ya kiroho na kimwili ya jumuiya yao.