Ufinyanzi uliotengeneza kwa ajili ya sherehe ya jumuiya Katika maandalizi kwa ajili ya sherehe za miaka mia mbili, jumuiya ya Wabahá’í wa Poroma Bolivia, ilitengeneza sanaa za ufinyanzi ambazo zitaoneshwa wakati wa sherehe yao. Watoto, vijana, na watu wazima walibumba kwa upendo vikombe, mitungi ya maua, na vifaa vingine katika shughuli hii ya kijumuiya.