close

Malaysia

Karamu ya kisanii iliyopambwa rangi ya Seremban, Malaysia
Kwa heshima ya Sherehe Pacha Takatifu za Kuzaliwa, jumuiya ya Wabahaí wa Seremban, Malayia, waliandaa sherehe ya kisanii katika Bahai senta ya Seremban. Yapata washiriki 110 walijumuika, ikijumuisha familia na wawakilishi kutoka mashirika ya mahali ya kidini. Sherehe ilijumuisha warsha iliyoendeshwa na msanii ambaye aliwahamasisha washiriki kuandaa michoro yenye mada ya umoja katika utofauti. Lilikuwa ni tukio la furaha ambalo liliendeleza upendo na umoja kati ya washiriki, ambapo wengi kati yao walishiriki katika mazungumzo kuhusu mafundisho ya Bahaú'llah na shughuli za ujengaji jumuiya.