Jamii za jirani za nje ya Australia zasherehekea Jioni ya sala, muziki na sanaa, ilileta pamoja watu 70 kutoka jamii mbili huko Australia, akiwemo mmoja wa mameya, katika ukumbi wa manispaa. Jioni lijumuisha maonyesho ya sanaa kutoka kwa vijana na dansi maridadi iliyohuisha chumba kizima. Wageni walichunguza misheni ya Bab na Bahaullah, baadhi ya kanuni za Imani, na uwezekano wa kuongeza baadhi ya shughuli za kujenga jamii zinazoendelea katika ujirani wao.