close

Turkmenistan

Jamii yajiandaa kwa sherehe za miaka mia mbili
Katika kufikia sherehe za miaka mia mbili, watoto, vijana na watu wazima huko Ashgabat, Turkmenistan walikuwa wakiandaa sherehe zao. Kikundi cha marafiki kilikusanyika kusoma na kujifunza dondoo kutoka Maandiko Matakatifu ya Imani ya Kibahai, pamoja na barua kutoka Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, kabla ya kujadili ni aina gani ya shughuli wangeandaa kwa ajili ya sherehe zao. Vijana wadogo pia wamekuwa wakifanya mazoezi ya nyimbo na kutengeneza kazi za sanaa, ambazo zilijumuisha mabango yanayoonyesha historia ya Imani ya Kibahai katika nchi na picha za shughuli zinazoendelea za kujenga jamii