close

India

Jamii yaungana kujenga senta ya Kibahai kufikia kwenye sherehe za miaka mia mbili
Jamii ya kijiji cha Bramhapara, India, imejenga jengo wakitumia vifaa vya kienyeji kukaribisha michakato ya elimu ya watoto na vijana. Vijana wadogo katika jamii walishiriki katika mchakato wa nguvu wa elimu unohusisha umri tofauti katika mpangilio wa mafunzo na matendo wenye lengo la kuchangia katika maendeleo ya vitongoji vyake. Jengo lilizinduliwa na wajumbe wa jamii ya kijijini katika mkutano wenye shauku na wa heshima.