close

Azerbaijan

Binti wa Jua, igizo kuhusu Tahirih, lililoigizwa huko Baku
Kikosi cha waigizaji vijana walijitolea onyesho la mwaka huu la igizo kuhusu Tahirih kwa sherehe za miaka mia mbili za kuzaliwa kwa Bab. Binti wa jua ilionyeshwa kwanza huko Baku, Azerbaijan, mwaka jana na lilihusisha ushujaa wa mwanamke wa kwanza muumini wa Bab. Takribani watu 340 walitazama igizo hilo liliogusa na kuwezesha. Baadhi ya watazamaji baadae waliongelea kuhusu umuhimu wa ujumbe wa igizo hilo kwa dunia leo.