Sanaa za kudarizi zilizohamasishwa na uzuri wa Kaburi la Báb Kikundi huko Afrika Kusini kiliandaa kitambaa kilichofumwa cha ukutani kilichotengenezwa na vipande vyenye mishono ya kudarizi vilivyohamasishwa na uzuri wa Kaburi la Báb. Kitambaa kizima kitaonyeshwa katika maonyesho ya sanaa katika Kituo cha Kitaifa huko Johannesburg wakati wa sherehe za miaka mia mbili.