Maonesho yahuishwa huko Bali, Indonesia Maandalizi yanaelekea ukingoni kwa ajili ya maonesho juu ya maisha ya Báb huko Bali, Indonesia. Jumuiya ya Wabahá’í imeandaa maonesho yanayostahili ya picha yanayoonesha nyakati za kihistoria katika maisha ya Báb, yakiunganisha wageni kwenye kipindi Chake cha Utumishi kilichopita haraka na kilicho cha kusisimua.