Maonyesho ya vitu vya kihistoria vinavyohusiana na maisha ya Bab na Bahaullah Ndani ya siku 12, mamia ya watu walitembelea maonyesho huko Langenhain, Ujerumani, yakionyesha vitu vya ukweli vya kihistoria vinavyohusiana na maisha ya Bab na Bahaullah. Wahudhiriaji waliguswa na ukaribu wa Wadhihirishaji pacha ulionyeshwa wakati wa onyesho hilo. Katika kituo kimoja, kitabu, kilifunguliwa katika kifungu kilichoandikwa na Bab kuhusu Bahaullah, na kwingine, kwenye kifungu kilichoandikwa na Bahaullah kuhusu Bab. Baadhi ya vitu vingine katika maonyesho ilikuwa ni fungu la nywele za Miumbo Pacha Mitakatifu, nakala iliyoandikwa kwa mkono kutoka Kitabi-Aqdas, na mchapisho wa mhuri wa Bahaullah, vipande vya nguo ya Bab, kipande cha ukuta kutoka ngome ya ya Mah-Ku ambapo Bab alifungwa kwa miezi minane.