Maonesho ya kazi za sanaa anuwai Ikikumbusha taswira na sitiari za kina za maisha na ujumbe wa Báb, wasanii zaidi ya dazeni nchini Ireland walishirikiana kuandaa onyesho liloitwa “Milango”. Maudhui yake yalitokana na hadhi ya jina la Báb, ambayo maana yake ni Lango, na “yakikaribisha uchunguzi wa kina wa mawazo mipaka na mabadiliko; mwanzo na mwisho; uhusiano kati ya ulimwengu wa kimwili na ulimwengu wa kiroho.” Maonyesho yalijumuisha picha za rangi, michoro, kazi au sanaa za ufinyanzi, na nyingine zaidi zilizohamasishwa na maudhui haya.