close

Argentina

Mtazamo wa sherehe pande zote za nchi
Katika jiji la Berisso, Argentina, watoto, vijana na watu wazima walisherehekea sherehe za miaka mia mbili katika mazingira ya furaha na umoja .Huko Salta, watoto walitengeneza michoro iliyotokana na vifungu na kutengeneza orofa ya sanaa. Katika sehemu nyingine za nchi, ubunifu wa kisanii ukiwemo mapambo ya maua, michoro ya rangi, sala zilizowekwa katika muziki, na video inayoelezea kwa ufupi historia ya Bab na kuelezea matokeo ya ujumbe Wake Argentina na duniani kote.