Heshima iliyofanywa na mji ambao uliandaa marumaru zilizotumika katika ujenzi wa Makao Makuu ya Wabaha'i Sherehe huko Chiampo, Italy, zilizowaleta pamoja zaidi ya watu 200 katika mkusanyiko ambao ulitoa heshima kwa mchango uliofanywa na wazalishaji marumaru wa hapo mjini. Kampuni la Margraf ya Chiampo ilizalisha marumaru ambazo zilitumika katika ujenzi wa Makao Makuu ya Wabaha'i na Nyumba ya Ibada ya New Delhi, India. Walioshiriki waliguswa na masimulizi ya mafundi waliostaafu ambao walisaidia na uandaaji wa vipande hivyo na pia maonesho yaliyojumuisha mawasiliano kati ya Makao Makuu na kampuni hiyo.