close

Kenya

Marekebisho kwenye senta ya Kibahai iliyojengwa tangu maadhimisho yaliyopita ya miaka mia mbili
Huko Kariene, Kenya, jamii inaimarisha jitihada zake toka sherehe za miaka mia mbili zilizopita. Mnamo mwaka 2017, wakati wa sherehe za miaka mia mbili za kuzaliwa kwa Bahaullah, lango jipya la kuingilia ndani ya senta ya Kibahai lilijengwa. Mwaka huu, wanajenga bweni. Sehemu mpya itawahifadhi wageni wanaolala ambao mara kwa mara hutembelea kwa ajili ya michakato inayohusiana na jitihada za kielemu zilizohamasishwa na Ubahai.