Usiku wa sherehe za furaha huko Sheffield, Uingereza Watu wa kila umri na usuli walikusanyika kwa pamoja huko Sheffield, Uingereza, kwa usiku uliochangamshwa wa sala, muziki na majadiliano kuhusu maendeleo duniani zaidi ya miaka 200 iliyopita kuhusiana na mafundisho ya Báb na Bahá’u’lláh.