Gazeti lachapisha toleo maalum la sherehe za miaka mia mbili Jamii ya Wabahai wa Uingereza walichapisha toleo maalum la sherehe za miaka mia mbili la gazeti lake. Nakala zilizokusanywa kwa uangalifu na picha zilitoa maelezo kuhusu maisha ya pekee ya utotoni ya Bab, nyakati za kihistoria katika historia ya dunia wakati wa utume Wake, na watu walioishi katika kipindi Chake.