close

New Zealand

Nembo ya miaka mia mbili ya Māori
Huko New Zealand, nembo ya miaka mia mbili lilisanifiwa kwa mtindo wa Kimaori unaoitwa kowhaiwhai. Nembo inatumia mtindo wa kowhai ngutukaka-ambao huashiria mazungumzo, jumuiya na mwanzo mpya-na mtindo wa mangopare ambao huashiria uwezo na nguvu. Nembo yenyewe kwa pamoja, huwakilisha jua linalochomoza alfajiri, likiongelea ujio wa Bab kama Mdhihirishaji wa Mungu.