Msukumo wa kasi wajengwa kuelekea sherehe huko Athens Jamii huko Athens, Ugiriki, walianza maandalizi ya sherehe za miaka mia mbili kwa kukutana kufikiri juu ya jinsi gani watakaribisha marafiki kusherehekea tukio hili lenye umuhimu mkubwa. Baadhi ya marafiki waliongeza nguvu kwenye mafunzo yao ya mafundisho ya Bab wakati wengine walifanya mikutano midogo ya ujirani kutafakari juu ya maisha Yake. Onyesho maalum la filamu ya Mwanga wa Alfajiri lilifanywa katika sehemu nyingine ya mji na majadiliano ya kina yalifuatia. Katika matukio yote, wale waliokusanyika walivutwa kuwaalika marafiki zaidi kwenye sherehe za miaka mia mbili zilizofanyika katika jengo la manispaa.