Sanaa za kazi za picha zilizopangwa kwa mawe kutoka Colombia Kikundi cha Wabahai wa Bogota walihamasishwa na hali ya kiroho ya tukio kuandaa mradi was sanaa, huko Bogota, Colombia. Vipande tofauti vya sanaa vilitengenezwa ili vitumiwe katika sherehe za miaka mia mbili. Watu binafsi wa kila umri walishirikiana katika utengenezaji wa sanaa tofauti.