Muziki uliohamasishwa na sala na maandiko kwa Kirusi Makundi matatu ya wanamuziki kutoka maeneo mbalimbali huko Urusi wamerekodi nyimbo zilizohamasishwa na sala za Kibahá’í na maandiko. Wanamuziki kutoka St. Petersburg, Perm, na Ulan-Ude wote wamechangia muziki kwenye albamu ambayo Baraza la Kiroho la Kitaifa la Urusi liliagiza itengenezwe kwa heshima ya sherehe za miaka mia mbili.