close

Uingereza

Tukio la muziki lasherehekea hali ya uanuwai na sherehe za miaka mia mbili
Kusherehekea sherehe zijazo za miaka mia mbili na kutoa heshima kwa anuwai katika jamii, takribani watu 120 walikusanyika katika mji wa Blaina, Uingereza, kusherehekea kwa maonyesho ya muziki. Mkutano ulihudhuriwa pia na maafisa wa serikali ya kijiji. "Ni namna gani ya ajabu ya kuleta watu pamoja kwa roho ya upendo na umoja kwa kutumia nguvu ya muziki na nyimbo" mmoja wa wandaaji alisema.