Michoro kuhusu ufunuo uendeleao Maonesho ya Sanaa huko Portimão, Ureno, ukihusisha michoro kuhusu ujio wa kufuatana wa Wadhihirishaji wa Mungu, dhana ifahamikayo kama ufunuo uendeleao. Maonesho hayo yamewekwa kwenye Kituo cha Kibahá’í cha mahali hapo na pia yataoneshwa kwenye sehemu za umma kama vile jingo la halmashauri ya manispaa.