close

Ufaransa

Michoro ya rangi inayotoa tafakari ya mwelekeo wa kiroho wa maisha
Msanii kutoka Ufaransa alitenegeneza michoro ya rangi iliyohamasishwa na maandiko ya Kibahai. Ya kwanza iliitwa "mwanga wa umoja", ilihusu umoja wa dini. Ya pili "moto wa chuki", ilichunguza wazo la kuiishinda chuki kwa jitihada na sala. Ya tatu iliitwa "mlingano wa kuzaliwa", ilichunguza wazo la maisha ya kiroho. Mchoro wa rangi wa mwisho uliitwa "paradiso la bustani", ulitafakari katika wazo la safari ya milele ya roho kufikia ukamilifu.