Igizo kuhusu Táhirih lililofanyika kusini mwa Ufaransa Igizo hili kuhusu shujaa wa kike Táhirih lilichezwa kwa kipande kusini mwa Ufaransa na litaigizwa tena kwa ajili ya umati mchanganyiko kwenye nyumba za filamu huko Ufaransa na Uswizi. Igizo linaigiza kipindi cha mwisho cha maisha ya Táhirih wakati alipokuwa amefungwa na mwishowe kuuwawa kwa ajili ya imani yake kwa Báb na mafundisho Yake.