Sala ya ‘Abdu’l-Bahá katika lugha ya Kitonga Wakazi wa jamii tofauti katika visiwa vya Kaskazini waliimba sala inayojulikana vema ya ‘Abdu’l-Bahá katika lugha ya Kitonga. Sala hiyo, kwa Kiswahili, husema, "E Mungu, uniongoze, uninilinde, unifanye taa ing'aayo na nyota imulikayo. Wewe u Mweza na Mwenye Nguvu". Mkutano huu wa ibada ulikuwa ni sehemu ya mkusanyiko mkubwa ambapo kikundi kiliandaa kwa ajili ya sherehe za miaka mia mbili kupitia tafakari juu ya maendeleo ya mchakato wa elimu wa nguvu unaofanyika katika jumuia zao, ambapo watu wa umri tofauti wanajihusisha katika mfumo wa mafunzo na matendo yenye lengo la kuchangia katika maendeleo ya ujirani wao.