Sala Katika eneo la Nyumba ya Ibada ya Papua New Guinea Sala na muziki zilihamasisha washiriki wa mkutano wa ibada uliofanyika katika eneo litakalojengwa Nyumba ya Ibada ya Kibahá’í mjini Port Moresby, nchini Papua New Guinea. Kwa heshima ya miaka mia mbili ya kihistoria, vijana kwenye mkusanyiko huo pia walitoa uwasilisho juu ya maisha ya Báb.