Maonyesho ya filamu ya Alfajiri ya Mwanga yahamasisha pande zote za Uingereza Filamu Alfajiri ya Mwanga imekuwa ikonyeshwa kwa upana katika matukio pande zote za Uingereza. Filamu inachunguza ujumbe unaohuisha wa Bab na matokeo yake katika jamii hivi leo ikiwemo suala la kujitambua na uwezeshaji wa kimaadili na kiroho. Baadhi ya matukio haya yalisaidiwa na maonyesho kuhusu Bab, na mengine yalifuatiwa na jopo la majadiliano. Mkusanyiko mmoja huko Manchester ulihudhuriwa na idadi ya waheshimiwa wa kijiji pamoja na wawakilishi kutoka shule na jamii mbali mbali za imani.