Kikundi chatengeneza filamu fupi kuhusu shughuli za jamii kwa ajili ya sherehe za miaka mia mbili Kikundi huko Edmonton, Canada, kilitengeneza filamu fupi ikionyesha umaizi na uzoefu wa watu wachache wakifanya kazi kufikia kujenga jamii zenye shauku. Filamu inazingatia katika jitihada zinazolenga kuboresha hali za kiroho na kimwili za maisha za jamii na ikiwa na simulizi za wale wanaojihusisha na mchakatu huu.