Wimbo kuhusu kujitangaza kwa Báb kama "Mwahidiwa" Wimbo huu ulivuta kutoka kwenye matamshi ya Báb wakati Alipojitangaza kuwa Mwanzilishi wa dini mpya itakayo andaa ulimwengu kwa ujio wa Bahá’u’lláh. "Mimi ndimi, Mimi ndimi, Mwahidiwa! Mimi ni yule Ambaye jina lake kwa miaka elfu moja mlilitaja...," yalikuwa ni matamshi yaliyosisimua ya Báb kwa wageni Wake katika usiku wa tarehe 22 Mei 1844. Uliopangiliwa na wanamuziki wa Uhispania, wimbo huo pia ulinukuu vifungu vingine kutoka kwenye maandiko ya Kibahá’í kuhusu Ujumbe uangazao wa Báb.