Nyimbo na maigizo yaliyopata uvuvio kutokana na kumbukizi ya miaka mia mbili Mkutano huko Mantova, Italia, ambapo watu kutoka nchi nzima walikuwa wamekusanyika ili kujadili maendeleo ya kiroho na ya kidunia ya jumuiya zao, ulihusisha maonesho ya kisanii yaliyopata uvuvio kutokana na kumbukizi ya miaka mia mbili. Mawasilisho yalihusisha sala za Kibahá'í ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye muziki, nyimbo zilizotungwa maalum kwa ajili ya sherehe za miaka mia mbili, na maigizo ambayo yalitokana na matukio yaliyoyazunguka maisha ya Báb.