close

Kiribati

Machwa huko Kiribati yalifungua sherehe za ulimwengu
Wakati jua likizama katika kisiwa cha Kiribati, sherehe za miaka mia mbili za kuzaliwa kwa Báb zimeanza rasmi. Katika mwaka huu wa kihistoria, sherehe Pacha za kuzaliwa kwa Báb na Bahá’u’lláh zitasherehekewa na mamilioni ya watu ulimwenguni kote katika saa 72 kutoka mchomozo wa kwanza wa jua hadi wa mwisho, na kumaliziwa huko Hawaii tarehe 30 Oktoba.