Maonyesho ya maigizo yajitokeza kutoka kwenye mafunzo ya Wavunjaji Alfajiri Kikundi cha vijana cha Bucharest, Romania, kimekuwa kikutana kujifunza kitabu cha Wavunjaji Alfajiri katika mwaka wa sherehe za miaka mia mbili. Baada ya kujifunza hadithi za mashujaa wa mwanzoni wa Imani kikundi kilivutwa na kutengeneza igizo. Kupitia maonyesho yao kikundi kilisherehekea hadithi za binti mdogo wa Kibabi, Zaynab, na kilichonguza dhana ya kuwa mtafutaji wa kweli kupitia hadithi ya Mulla Husayn